Tafadhali zingatia yafuatayo kabla ya kufanya Malipo kupitia TIGO PESA LIPA KWA SIMU
a. KANUNI NA MASHARTI
- Gharama ya kufanya malipo ya udahili ni Tshs 15,000/- na si vinginevyo.
- Tunapokea malipo kutoka mtandao wa Tigopesa kwenda TIGO LIPA KWA SIMU na si vinginevyo.
- Fedha ya Maombi itakayolipwa ikiwa imezidi au kupungua kiwango tajwa hapo juu haitorudishwa.
- Baada ya kufanya malipo hayo muda mchache sana utapokea ujumbe kupitia namba ya Tigo iliyotumika kufanya malipo, ujumbe huo wenye code zenye mfanano na MSICT2311(Verification code) ambazo utazitumia ili kuendelea kufanya maombi ya chuo.
- Unakumbushwa kusoma vigezo na sifa kwa waombaji wa kozi husika kwani fedha haitorudishwa kama itatokea umekosa nafasi.
- Unashauriwa kama hauna namba ya Tigo ni bora ukaazima ya mtu ili ikusaidie kufanya malipo uweze kupata code za maombi.
b. JINSI YA KULIPIA
- Bonyeza *150*01# kupata Menu ya TIGOPESA
- Chagua namba 5 Lipa Kwa Simu
- Kisha namba 1 Kwenda Tigo Pesa
- Ingiza Lipa namba
15091269
- Ingiza kiasi cha kulipa
15,000/=
- Ingiza namba ya siri ya tigopesa kutuma Tsh 15,000/= kwenda MILITARY SCHOOL OF ICT .
IMETOLEWA NA:
OFISI YA UDAHILI
SHULE YA KIJESHI YA TEHAMA (SKT)
Tarehe ya mwisho ya kufanya Approval ya kutoka NTA4 kwenda NTA5 na NTA5 kwenda NTA6 ni tarehe 25 September 2024.